Thursday, July 21, 2011

Jairo asimamishwa kazi

Best Blogger Tips
Via Uhuru

SERIKALI imemsimamisha kazi Katibu Mkuu  wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.  Hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya   ufanyika uchunguzi dhidi ya tuhuma  zinazomkabili zilizoibuliwa bungeni.

Jairo anadaiwa kuziandikia barua idara na  taasisi zilizo chini ya wizara ili kila moja itoe  sh. milioni 50 kwa ajili ya kufanikisha  uwasilishaji wa makadirio ya matumizi ya  wizara kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Anadaiwa pia kuwalipa posho za safari  watumishi wa wizara waliofuatana na  viongozi wa juu licha ya kuwa walishalipwa  na idara na taasisi zao.

Wabunge Beatrice Shellukindo (Kilindi-CCM)  na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro  -CCM), ndio walioibua tuhuma hizo  walipojadili makadirio ya wizara, kabla ya  serikali kuyaondoa bungeni.  Serikali iliyaondoa makadirio hayo bungeni  kutokana na hoja za wabunge kuwa  haijajipanga kukabiliana na tatizo la umeme.  Bunge limetoa wiki tatu kwa serikali  kujipanga na kuyarejesha.

Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo,  akizungumza na waandishi wa habari jana  mjini hapa, alisema amemwagiza Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG), kufanya uchunguzi wa kina, ambao  anatakiwa kuukamilisha ndani ya siku 10  kuanzia alipopewa kazi hiyo. "Wakati uchunguzi ukiendelea, Jairo   mesimamishwa kazi.

Hatua nyingine  zitafanyika baadaye kulingana na matokeo  ya uchunguzi," alisema. Luhanjo alisema anatarajia kufanya uteuzi  wa mtu atakayekaimu nafasi hiyo katika  kipindi kisichozidi siku tatu. Luhanjo alisema baada ya uchunguzi  kukamilika na endapo tuhuma dhidi ya Jairo  zitathibitika, uamuzi dhidi yake utachukuliwa  na rais kwa kuwa ndiye mamlaka yake ya  uteuzi.

Alisema amachukua uamuzi huo dhidi ya  Jairo kwa kuwa sheria ya  tumishi wa  umma inampa uwezo wa kushughulikia  nidhamu serikalini. "Kwa sababu suala hili ni zito nimeamua  aende likizo, lakini baada ya uchunguzi na  nikipata matokeo ya uchunguzi huo nitampa  taarifa itakayoambatana na hati ya  mashitaka," alisema. Akizungumzia utaratibu alisema baada ya  matokeo ya uchunguzi kupatikana, Jairo  atapatiwa taarifa itakayoambatana na hati  ya mashitaka, itakayoeleza kwa kifupi kosa  alilotenda na namna alivyolitenda ili atoe  majibu.

Luhanjo alisema katika kipindi hicho,  atakuwa amesimamishwa kazi na kuanza  kulipwa nusu mshahara.  Kwa mujibu wa Luhanjo, katika majibu,  anaweza kukubali au kukana tuhuma dhidi  yake, ambapo mamlaka ya nidhamu  itaendelea kutoa adhabu kulingana na uzito  na kwamba, kwa kuwa Jairo ni mteule wa  rais, ndiye atakayeamua hatima dhidi yake.
Endelea kusoma habari hii...............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits