Monday, July 25, 2011

Gamba laivuruga CCM

Best Blogger Tips
 Nape Nnauye

MPANGO mkakati wa kujivua gamba kwa lengo la kurejesha uhai ndani ya CCM unaelekea kuwa bomu la maangamizo kwa chama hicho, baada ya baadhi ya wenyeviti wa mikoa kuupinga huku wakiagiza wafuasi wao kuwashusha majukwaani makada wanaoupigia debe.Wakati wenyeviti hao wakiupinga, Baraza Kuu la Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), jana limetoa tamko rasmi la kuunga mkono ziara hizo zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa chama hicho, Nape Nnauye za kutekeleza mkakati huo.

Mpango huo wa kujivua gamba ulitangazwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa chama hicho kikongwe barani Afrika, lakini jana baadhi ya wenyeviti wake wa mikoa akiwamo, John Guninita wa Dar es Salaam na Hamis Mgeja wa Shinyanga, waliupinga wakisema unamwaga sumu kali dhidi ya chama.

Msimamo wa UVCCM

Baraza Kuu la UVCCM limetoa msimamo wake kuunga mkono ziara za mikoani zinazoongozwa na Nnauye za kujivua gamba huku likiweka bayana kuwa huo ni msimamo wa Halmashauri Kuu (Nec) ya chama na si wa Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi.

Mbali na Nape, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wamekuwa wakifanya ziara mikoani hasa katika mwisho wa wiki ambazo pamoja na mambo mengine, wamekuwa wakifanya mikutano ya kukipa uhai chama huku wakitangaza uvuaji gamba.

Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa alisema UVCCM ilipongeza uamuzi wote wa NEC: "Kila kinachofanyika ni sahihi na sisi tunaunga mkono kabisa."
Endelea kusoma habari hii.................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits